Ijumaa 3 Aprili 2026 - 12:30
Utawala haram wa Israel ufikishwe mahakamani kutokana na uhalifu walioupanga dhidi ya wanahabari na watu wa huduma ya kwanza

Hawza/ Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama nchini Lebanon, umetangaza kuwa; unatoa hukumu kali na chuki kubwa dhidi ya uhalifu wa aibu uliotekelezwa na jeshi la utawala haram wa Israel dhidi ya jamii ya vyombo vya habari nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama katika taarifa yake ulitangaza hukumu kali na chuki kubwa dhidi ya uhalifu wa aibu uliotekelezwa na jeshi la utawala haram wa Israel dhidi ya jamii ya vyombo vya habari nchini Lebanon; ambapo wanahabari (Ali Shuaib, Fatima Fatuni na Muhammad Fatuni, kutoka Luninga za Al-Manar na Al-Mayadeen) waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kitaaluma walilengwa kwa makusudi na kwa mpango uliotayarishwa mapema.

Umoja huo ulisisitiza kwamba; kulengwa kwa wanahabari na timu za matibabu kusini mwa Lebanon si tukio la muda mfupi linaloweza kutenganishwa na muktadha wa jumla, bali limegeuka kuwa mwenendo unaojirudia ambao unakumbusha matukio ya vita vya Ghaza; mahali ambapo makundi yaliyo chini ya ulinzi wa sheria za kimataifa za kibinadamu yaligeuzwa kuwa malengo ya moja kwa moja.

Umoja wa wanazuoni uliongeza kwamba: Sisi, pamoja na kulaani mauaji haya ya wanahabari na mlolongo wa mashambulizi yaliyotangulia dhidi ya timu za vyombo vya habari na matibabu, tunaona kinachoendelea kuwa ni uhalifu wa kivita uliothibitishwa ambao haupotezi muda wake wa kisheria (haupitiwi na muda) wala hauwezi kufutwa kwa kisingizio chochote.

Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama ulisisitiza kwa kusema: Tunaiomba jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za haraka kuufikisha mahakamani utawala haram Israel, kwa sababu ya kutekeleza uhalifu uliopangwa dhidi ya wanahabari na wahudumu wa uokoaji, na isijitosheleze kwa kutoa taarifa za kulaani zisizo na athari. Pia tunaziona nchi zinazounga mkono utawala huu, hasa Marekani, kuwa zinawajibika kikamilifu kwenye uhalifu huu kutokana na ulinzi wa kidiplomasia unaoendelea, usambazaji wa silaha na uungaji mkono wake kwa utawala huu. Aidha, tunataka mashambulizi yote ya Israel dhidi ya timu za vyombo vya habari na matibabu nchini Lebanon yachunguzwe ndani ya mfumo wa uchunguzi huru wa kimataifa, na matokeo yake yawasilishwe kwenye mahakama za kimataifa zenye mamlaka husika.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha